Thursday 21st, November 2024
@
Katika kutambua dhana na umuhimu wa Utawala Bora Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wameandaa na kuratibu mafunzo yenye malengo ya kuendelea kuwajengea uwezo, kuboresha masuala yanayohusu uongozi na kuimarisha utawala Bora kwa Viongozi wa ngazi za Wilaya, Mkoa wa Kagera.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Chuo cha Uongozi cha Dar es salaam na washiriki wa mafunzo haya ni wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kagera.
Kwa upande wa Wilaya ya Muleba, mafunzo hayo yamehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Mhe. Magongo Justus,Katibu Tawala wa wilaya ya Muleba, Ndg. Greyson Mwengu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila.
Ni Mafunzo ya Siku tatu Kuanzia tarehe 18-20/11/2021 na yanafanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa