Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Muleba umepokelewa tarehe 29/09/2024 katika kiwanda cha Samaki cha pride of Nile Limited kilichopo katika kata ya Izigo,ukitokea katika Manispaa ya Bukoba na kukagua Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika sekta ya Elimu,Afya,Mazingira,Maji na Barabara yenye thamani ya shilingi Bil 8.1.
Miradi iliyotembelewa na mwenge wa uhuru kwa mwaka 2024 ni Mradi wa Kiwanda cha samaki cha Pride of Nile Limited wenye thamani ya Shilingi Bil.5, Mradi wa Shamba la Kahawa la Vijana katika kijiji cha Makongora wenye thamani ya shilingi Mil 97.5, Mradi wa ujenzi Shule ya Sekondari Makongora iliyogarimu kiasi cha shilingi Mil. 643, Mradi wa Kitalu Cha Miti Mafumbo wenye thamani ya shilingi Mil. 550, Mradi wa kituo cha afya Buganguzi uliogarimu kiasi cha shilingi. Mil 309, Mradi wa tenki la maji Kishanda lililogarimu kiasi cha shilingi Bil 1.2, pamoja na ujenzi wa barabara ya Marahala-MSD yenye urefu wa Kilometa 0.4 uliogarimu kiasi cha shilingi Mil.193.
Akizungumza Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Ndugu Godfrey Eliakimu Mzava, kwa nyakati tofauti baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo, amesema miradi yote ambayo imepitiwa na mwenge imetekelezwa kwa kiwango kinachoridhisha na kuwataka kuitunza miradi hiyo kwa manufaa ya Taifa endelevu.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndugu Godfrey Mzava akiwa katika Kiwanda Cha Samaki Pride of Nile Limited ameutaka uongozi wa Kiwanda hicho kuhakikisha kabla ya mwaka huu kinaanza kutoa huduma kwa lengo la kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la Samaki katika sekta ya uvuvi ili kuinua wananchi kiuchumi.
Aidha,Kiongozi wa mbio za mwenge akiwa katika shamba la Vijana la kahawa Makongora amempongeza Mkuu wa Mkoa Mhe.Hjjat Fatma Mwassa Kwa juhudi kubwa ya kutekeleza sera ya vijana kwa kuanzisha Mradi mkubwa wa Shamba wenye lengo la kutoa fursa za ajira kwa Vijana wa Muleba na kuchangia pato la Wilaya na Taifa.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa