Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera limepitisha kwa kishindo taarifa za hesabu za mwisho za mwaka wa fedha 2023/2024.
Baraza hilo limepitisha taarifa hiyo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kujadili na kupitia taarifa za mwisho za hesabu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambacho kimefanyika September 24 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Awali akiwasilisha taarifa hiyo Mweka hazina Mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Muleba, ndugu Yona Charugamba ameomba ushirikiano katika ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufikia lengo la makusanyo lililokusudiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe.Magongo Justus amewashukuru na kuwapongeza watalaam wa Halmashauri kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika kutekeleza majukumu ya kazi na kupelekea kupata hati safi hivyo amewataka kuendelea kutoa ushirikiano na kujituma zaidi ili kuepuka hati chafu katika halmashauri.
Aidha Baraza la madiwani limeipongeza halmashauri kwa kutimiza matakwa ya kisheria ambayo yatapelekea kupata hati safi kwani hadi kufungwa kwa hesabu za mwaka,jumla ya shilingi bilioni 10.686 zimekusanywa ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa