Shirika la Wazee Nshamba limekuwa msaada mkubwa sana kwa wazee wa wilayani Muleba wenye umri wa kuanzia miaka 70 ambapo wazee hao wamekuwa wakipata huduma mbalimbali ikiwemo malipo ya Pensheni, Mazoezi ya viungo na huduma za kiafya.
Moja ya majukumu ya Shirika hili ni kuwa huduma wazee kiafya ambapo umpeleka Daktari katika maeneo yao kwa ajili ya kufanya uchunguzi na wagonjwa wanaobainika hupewa matibabu kulingana na matatizo wanayokutwa nayo ikiwemo kufanyiwa operesheni.
Dkt. Lwabukambwe Emmanuel, Daktari wa Macho katika hospitali ya Ndolage, iliyopo kata Kamachumu, Wilaya ya Muleba ameeleza kuwa Presha ya Macho, mtoto wa jicho na ukungu wa macho ni magonjwa yanayowakabili wazee wengi hivyo kushindwa kujitegemea/kujihudumia wenyewe. Baada ya kulitambua hilo Shirika la kwa Wazee Nshamba liliona umuhimu wa kuwahudumia wazee kwa kuwagharamia matibabu hayo ambapo hatua za awali madaktari wanakwenda katika kijiji husika na kufanya uchunguzi na vipimo, baada ya hapo wazee wanaogundulika na matatizo mbalimbali hupewa matibabu mbalimbali kama vile dawa, miwani na upasuaji.
"Mwanzoni huduma hii ilikuwa inatolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kupitia Idara ya Afya, kifungu cha mfuko wa" Basket Fund" lakini baada fedha hizi ziliachwa kutolewa na wafadhili ndipo Shirika la Wazee Nshamba liliona umuhimu wa kuendeleza huduma hii muhimu kwa wazee wetu" alieleza Dkt. Lwabukambwe Emmanuel.
Changamoto kubwa wanayokutana nayo wakati wa matibabu na wazee kuwa na magonjwa mengine kama Kisukari, matatizo ya moyo, mifupa na presha hivyo kuchukua muda mrefu kuwatibu lakini shirika limekuwa likiwadumia wazee hao kwa magonjwa yote wanayobainika kuwa nayo hadi wanapona au kupata nafuu.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa