Shirika la (KOICA) kutokea Nchini Korea Kusini lenye matawi yake Barani Afrika kwa kushirikiana shirika la (LVRLAC) lililopo Mwanza wametoa ufadhili wa Taa kwa Wavuvi Wilayani Muleba ili kuweza kuwasaidia kuboresha shughuli zao za uvuvi pamoja na kuongeza pato lao.
Akizungumza katika hafra ya uzinduzi wa mradi huo Mkurugenzi wa Shirika la KOICA Mr.Shin amesema kuwa mradi huo wa Taa za nishati ya jua zitakazotumiwa na wavuvi umegharimu kiasi cha Tsh.milioni 29.7.
Aidha, amelipongeza shirika la (LVRLAC) kwa ushirikiano walioutoa kwa kuweza kutoa fedha zinazofikia kiasi cha dolla 2500 kwa ajili ya kupanga na kutekeleza mradi huo.
Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la (KOICA) Kwang IK Park ameeleza kuwa alifanya utafiti na kuja na mbinu mpya ya kuweza kutunza na kulinda raslimali za ziwa kwa kutumia taa za nishati ya jua kufanya shughuli za uvuvi wa Dagaa.
"Matumiza ya taa za nishati ya jua zitasaidia katika uhifadhi wa ziwa na kumnufaisha mvuvi kichumi kwa mda mrefu" amesema Kwang IK Park.
Naye Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Muleba Ndg. Wilifred Tibendelana amewaeleza wavuvi kulilinda ziwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha na uvuvi endelevu hasa kwa kulinda na kutunza ziwa bila ya kujihusisha na Uvuvi haramu ambao unaweza kupelekea uharibifu wa ziwa jambo ambalo linaweza kusababisha kutokuwepo kwa uvuvi endelevu.
Ndg. Abel Costantine ambaye ni mmoja Wa wavuvi wa dagaa amesema kuwa taa hizi zitaweza kuwasaidia katika shughuli zao za Uvuvi kwa sababu hapo awali taa walizokuwa wanazitumia walikuwa wakikumbana na changamoto ya upotevu wa betri ambazo zilitumika kuwashia taa hizo lakini kupitia taa hizi ambazo zinachajiwa zitawasaidia kuondokana na changamoto hizo.
Shirika la (KOICA) kwa kushirikiana na Shirika la (LAVRLAC) wametoa jumla ya Taa 40 kwa wavuvi ambazo watazitumia kwa kipindi cha majaribio ya mda wa mwezi mmoja bila malipo na baada ya hapo kwa mvuvi ambaye atakuwa tayari kuendelea kutumia taa hizo ataweza kununua na kumiliki taa hizo moja kwa moja.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa