Katika mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu baina ya Watumishi wa Halmashauri na Madiwani wa wilaya ya Muleba Watumishi wamefanikiwa kuifunga timu ya Madiwani bao 1-0 na kuibuka washindi wa mchezo huo uwanja wa CCM Muleba.
Mgeni rasmi wa mchezo huo Mkuu wa wilaya ya Muleba ametoa pongezi kwa timu zote mbili kwa uwezo waliouonesha katika mechi hiyo na kushauri kuundwa kwa timu ya wilaya ya Muleba kwa kuanza kutafta watu wenye uwezo kuanzia ngazi ya Kata ili wilaya iweze kuwa na timu itakayoweza kushiri hata ligi kuu.
"Nimeona sasa kuwa ipo haja ya kuundwa timu bora ya wilaya ya Muleba ambayo itaweza kushiriki michezo mbalimbali hata kufikia kushiriki ligi kuu lakini pia tuanze kuwa na michezo mbalimbali kama kukimbia mbio ndefu na fupi, mchezo wa mpira wa kikapu pamoja na timu ya mpira wa miguu ya wanawake"amesema Mhe. Toba Nguvila.
Aidha, Mkuu wa wilaya amependekeza kuwepo kwa mwendelezo wa michezo hiyo ili kuweza kuimarisha ushirikiano na mshikamano baina ya watumishi na Waheshimiwa madiwani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Magongo Justus ametoa pongezi kwa timu zote kwa uwezo na umahili waliouonesha katika mchezo huo.na kumpongeza mlinda mlango wa timu ya Mhe. Muhaji Bushako kwa uwezo aliouonesha Katika mchezo huo.
Gori la timu ya watumishi ambao wameibuka wshindi katika mchezo huo limefungwa na Afisa Elimu Sekondari Mwl. Jared Muhile na kuipa timu ya watumishi ushindi wa bao 1-0
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa