Shirika la JSI, Kanda ya ziwa linalotekeleza mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya huduma za Afya Ngazi ya Jamii limetoa vitendea kazi, Kabati 11 na Baiskeli 33kwa wasimamizi wa wasimamizi wa Mashauri ya watoto, ngazi ya kata.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dr. Itros Sanga ameeleza kuwa lengo la kutoa vifaa hivi ni kusaidia kurahisisha kazi za wasimamizi wa shgughuli za watoto ili waweze kuwafikia kiurahisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Emmanueli Sherembi akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wasimamizi hao ameshukuru Shirika la JSI kwa kuona umuhimu wa kutoa vifaa hivyo ili kurahisisha utendaji kazi wa wasimamizi hao.
"Nawashukuru sana Shirika la JSI kwa kuona umuhimu wa kusaidia vifaa hivyo kwani wilaya ya Muleba ni kubwa na kufika kijiji hadi kijiji, inawalazimu wasimamizi hao kutembea umbali mrefu" alieleza Ndg. Emmanueli Sherembi.
Wasimamizi hao wameshukuru shirika la JSI kwa kuona umuhimu na kuwapatia vifaa hivyo kwa ajili ya kutunza nyaraka za mashauri hayo na kutembelea watoto wanaowasimamia.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa