Katika Ziara iliyofanywa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Wilayani Muleba Katika Kata ya Kamachumu alipotembelea na kukagua maendeleo ya shughuli za upanuzi wa Chuo cha (VETA) Ndolage amewahimiza wananchi Wilayani Muleba kuwapeleka vijana wao katika chuo hicho ili waweze kunufaika na elimu ya mafunzo ya ufundi Stadi.
Akizungumza Chuoni hapo Waziri Mkuu amesema kuwa kupitia mafunzo yanayotolewa katika Chuo hicho yataweza kuwasaidia vijana kupata ajira pamoja na kujiajili katika shughuli mbalimbali za kiufundi ambazo zitawawezesha kuwaingizia mapato na kusaidia kukuza uchumi wa Taifa.
"Hapa ndio mahali pa kupata ujuzi utakao tuongoza kufanya kazi za kiujuzi ambazo zitatuongezea Mapato binafsi na pamoja na Mapato ya Wilaya yetu na Taifa kwa ujumla, Chuo hiki kinaweza kuchukua vijana wa ngazi zote za Elimu ukiwa hapa kwa Taaluma yeyote ile unaweza kutoka na ujuzi wote wa kiufundi" amesema Mhe. Kassim Majaliwa.
Sambamba na hayo ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kutenga bajeti ya fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana wanaohitimu mafunzo ya ufundi Stadi kuwa na mitaji ya kuweza kuwasaidia kujiajili baada ya kuwa wamehitimu mafunzo.
Katika Taarifa iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (VETA) Ndg. Antony Kasore amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ilitenga na kutoa kiasi cha Tsh. milioni 903.57 kwa ajili ya kujenga na kuongeza miundombinu katika Chuo hicho.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa