Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu na Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) nchini Tanzania, Fred Kafero, wametembelea na kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika hilo liyoanzishwa mara baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi mwezi Oktoba,2016.
Wakiwa katika ziara hiyo wamefurahisha na utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo mradi wa ufugaji wa samaki, miradi ya viazi lishe na mihogo, mradi wa kilimo cha migomba na mradi wa ufugaji wa mbuzi wa maziwa.
"Nimefurahishwa sana na maendeleo ya mradi wa viazi lishe na mihogo katika kijiji hiki cha Nsambya na nina ahidi kuwasaidia kupata mashine za kusagia na masoko ya kuuza bidhaa zenu, " alieleza Mkuu wa Mkoa.
Aidha, katika ziara hiyo wameshiriki katika zoezi la upandaji migomba katika kijiji cha Kishanda, kata Kishanda.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa