Katika Mkutano uliofanyika Kata ya Kagoma Wilayani Muleba Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dkt Abel Nyamahanga amewasihi wananchi kujikita zaidi katika kilimo bora ili waweze kupata mazao yatakayowasaidia kuinuka kiuchumi na kuondokana na umaskini.
Akizungumza Katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya amewaeleza wananchi kuwa ni vema wakawatumia Maafisa Ugani ambao watawaelekeza namna bora ya kulima kitaalamu ili kuondokana na kilimo cha mazoea ambacho hakina utaalamu.
"Watendaji wa Vijiji shirikianeni na Maafisa Ugani kwenda kwa wananchi kutoa elimu ili waweze kulima kitaalamu na kupata mazao mengi yenye ubora yatakayowasaidia kunufaika zaidi na kilimo" ameagiza Mhe. Dkt Abel Nyamahanga.
Sambamba na hayo ametoa onyo kwa viongozi na watumishi wanaoshiriki katika vitendo vya uvuvi haramu na kuagiza wenye nyavu haramu kusalimisha nyavu hizo kabla ya hatua kari za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
Mkuu wa Sehemu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg. Charles Ntaki akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba amewaeleza wananchi kuwa suara la ushuru wa ndizi Halmashauri zote za Mkoa wa Kagera zilikubaliana kutoza kila mkungu wa ndizi kiasi cha Tsh. 500 hivyo kwa hakuna Halmashauri inayotoza ushuru tofauti na makubaliano hayo.
Katika Taarifa ya Kata iliyosomwa na Mtendaji wa Kata ya Kagoma Ndg. Lameck Chacha Ryoba amesema kuwa katika zoezi la kuendelea kupambana na uvuvi haramu tayari Kata ya Kagoma zimesalimishwa nyavu haramu aina ya timba 248 zenye thamani ya Tsh. Milioni 22.2 na kwa wale ambao hawajasalimisha kwa hiari mikakati imewekwa kuhakikisha wanafikishwa kwenye vyombo vya kisheria.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa