Katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi kilichofanyika ndani ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa ajili ya kampeni ya Kitaifa ya kutoa chanjo ya matone ya polio awamu ya nne Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba Ndg. Greyson Mwengu ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi ili watoto wao waweze kupatiwa chanjo hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba amesema kuwa chanjo hizo ni salama na zitatolewa kwa mda wa siku 4 kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 4/12/2022 na chanjo hizo zitawasaidia watoto waliopo chini ya miaka mitano kukua salama bila kushambuliwa na ugonjwa wa polio.
"Kama mzazi asipojitokeza kwa ajili ya mtoto wake kupatiwa chanjo hii ya polio anaweza akasababisha mtoto wake kushambuliwa na ugonjwa huu na sisi kama Serikali tusingependa kumpoteza mtoto yeyote kwa sababu ya ugonjwa huu wa polio na wakati chanjo tunazo" amesema Ndg. Greyson Mwengu.
Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa mpaka sasa Kamati ya Afya ya Msingi imeshajiandaa kuhakikisha zoezi hilo linakwenda vizuri na kwa viongozi wa kata na vijiji na vitongoji tayari wameshafikishiwa taarifa ili waweze kuwahamasisha wananchi zoezi hilo liweze kwenda vizuri.
Lakini pia ametoa rai kwa viongozi wa ngazi za chini kuhakikisha wanahamasisha wananchi ili waweze kujitokeza ili chanjo hii iweze kufanikiwa kwa asilimia ambazo zimepangwa na hata wao kama viongozi wamesisitiza kuhakikisha kila maeneo watakayopita watatoa elimu kwa wananchi ili zoezi liweze kufanikiwa.
MratibuwaChanjoyaPolioWilayayaMulebaNdg.Christinaamesemakuwaugonjwawapolioniugonjwaunaosababishwanavirusivyapolionaugonjwahusababishamtukupoozanahatimayekufariki.
Lakinipiaameongezakwakusemakuwavirusivyapoliohuingiamwilinikwanjiayamdomo,kwakunywamajiauchakulaambachokimechafuliwanakinyesikutokakwamtualiyeambukizwavirusihivyonaugonjwahuowapolioamesemakuwahaunatibabaliunawezakuzuiliwakwakupatachanjoyamatoneyapolio.
Kwa upande Evart Erenest Diwani wa Kata ya Rulanda amesema kuwa wao kama viongozi kwa ngazi za kata wameshajiandaa kuhakikisha kwamba wanawashirikisha makundi mbalimbali, watu mashuhuri, kwenye mikutano na hata kwenye magulio kuhakikisha kila mtu amepata ujumbe huu na kuuhakikisha kila mtu ametimiza wajibu huu wa watoto kupatiwa chanjo.
Naye Ndg. Johanes Mtoka mjumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi kwa upande wake ameeleza kuwa chanjo hiyo itaenda kusaidia watoto ambao wangeweza kupooza kwa kupata ugonjwa wa polio.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa