Maafisa Elimu ngazi ya wilaya na kata, Wakuu wa shule na walimu wakuu wamekutana na Kufanya kikao kazi cha pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila kwa lengo la kujiwekea mikakati katika kuongeza kiwango cha ufaulu kwenye sekta ya elimu.
Akizungumza na walimu hao, Mkuu wa wilaya ya Muleba, Mhe. Toba Nguvila ameeleza kuwa kipaumbele chake ni elimu hivyo amewataka walimu hao kuongeza kiwango cha ufaulu na kuwahaidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu ikiwemo uhaba wa miundombinu, changamoto za kiutumishi, maslahi yao na motisha.
" Naagiza kuanzia leo kuwepo na dirisha rasmi la kuwahudumia walimu wanapofika makao makuu ya wilaya na wapewe kipaumbele cha kusikilizwa ili wasitumie mda mwingi wilayani na kurudi kuwahudumia wanafunzi mashuleni" ameagiza Mhe. Toba Nguvila.
Katika kuwapa motisha walimu ili kuongeza kiwango cha ufaulu Mhe. Toba Nguvila ameeeleza kuwa hatuwezi kufanya vizuri bila kuwa na mikakati, amewahaidi kuongeza zawadi na kuanza kuwapa walimu watakaofaurisha vizuri katika masomo zawadi za viwanja ili kuzidi kuwatia moyo.
Sambamba na hilo Mhe. Toba Nguvila amehaidi kuanza matumizi ya TEHAMA shuleni kwa kutoa kompyuta kwa shule za Sekondari na Msingi na kwa kuanzia kwa muda wa mwezi mmoja wa utekelezaji wa majukumu yake wilayani Muleba tayari kuna shule nne mtaalamu amekuja na kubaini uhitaji wa vifaa hivyo na wakati wowote shule hizo zitapokea vifaa.
Wakitoa maoni yao walimu wameomba kuboreshewa miundombinu ikiwemo vyoo, madarasa na vyumba vya madarasa.Wialaya ione namna ya kuanzisha mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kuja shuleni.
Elimu iendelee kutolewa kwa wazazi ili kuongeza mwamko wa elimu na kudhibiti utoro utoro mashuleni. Pia wameomba kuendelea kupewa fursa za kozi mbalimbali ili kuendana na hali halisi.
Aidha, Mhe. Toba Nguvila ameeleza katika kuunga mkono jitihada zake Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amemuhaidi komyuta 10 kwa ajili ya shule zitakazoanzisha madarasa ya kompyuta.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Kishoju na kuhudhuriwa na walimu wakuu na wakuu wa shule wapatao 242 wa shule za msingi na sekondari, wa shule za Serikali na binafsi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Halmashuri ya wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa