Katika hafra fupi ya makabidhiano ya ofisi iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Dkt. Peter Nyanja amewahimiza Wakuu wa Idara na Vitengo kuwa wasimamizi bora wa miradi ya maendeleo ili utendaji kazi wao uweze kuonekana kuwa wa viwango vinavyostahili.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya ofisi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba amewaeleza Wakuu wa Idara kuwa utendaji wao wa kazi unapimwa kwenye miradi ya maendeleo hivyo amewaomba kushirikiana ili kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo imetekelezwa kwa ubora na kwa viwango vinavyostahili.
"Niwaombe sana Wakuu wa Idara tuwe wawazi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo tusimamie vyema na kuhakikisha tunazingatia ubora unaostahili katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba" amesema Dkt. Peter Nyanja.
Lakini pia amewasihi wakuu wa Idara kuwatendea haki watumishi wadogo ikiwa ni pamoja na kuwapa sitahiki zao kama inavyostahili.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amemueleza Dkt. Peter Nyanja kuwa tayari Halmashauri ilikuwa na mpango kwa bajeti inayofata kuhakikisha jumla ya madiwani 57 ambao bado hawajapata vishikwambi kununuliwa vishikwambi ambavyo watavitumia katika uendeshaji wa vikao vya Halmashauri ili kuweza kuondokana na mfumo wa zamani wa kutumia makabrasha katika uendeshaji wa vikao.
Sambamba na hayo amewashukuru waheshiwa Madiwani pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi cha utekelezaji wa majukumu yake alipokuwa Muleba na kuwasihi kumpa ushirikiano Dkt. Peter Nyanja Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa sasa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa