WAKUSANYA MAPATO WAHIMIZWA KUFANYA KAZI YAO KWA UBORA NA KWA KIWANGO KINACHOSTAHILI.
Katika zoezi la kuwasainisha upya mikataba wakusanya mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba baada ya kumaliza mkataba wao waliousaini tarehe 31/01/2022 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justus amewasihi kufanya kazi yao kwa ubora zaidi ili kuyafikia malengo ya Halmashauri.
Akizungumza wakati wa kusaini mikataba hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri amewasisitiza wakusanya mapato kuacha tabia ya kuwa wanawaachia mashine za kukusanyia mapato watu ambao hawahusiki na kazi hiyo.
"Mtu umekabidhiwa mashine lakini unampa mtu mwingine na unakuta sisi viongozi hatuna hizo taarifa hizo mashine sio simu ni kifaa ambacho tunakitumia kwa manufaa ya wananchi wa Muleba sasa wewe unachukua unampa mtu mwingine ambaye huna dhamana naye huo sio utaratibu wetu" amesema Mhe. Magongo Justus.
Aidha, amewasihi wadhamini wa wakusanya mapato kuhakikisha wanawahimiza wakusanya mapato kufanya kazi yao kama inavyostahili ili kuepuka kuwajibika endapo mkusanya mapato akikiuka utaratibu wa kazi yake.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amewasihi kila mkusanya mapato kuhakikisha anasimama kwenye nafasi yake ili mapato ya Halmashauri yaweze kuongezeka zaidi na kuyafikia malengo ya Ukusanyaji wa Mapato ambayo Halmashauri imejiwekea.
Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa