Katika hafra ya uzinduzi wa Makala ya Utekelezaji wa Miradi kwa kipindi cha Miaka Miwli ya Mhe. Dr Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Muleba Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba Ndg. Greyson Mwengu akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amewasihi Viongozi kufanya kazi kwa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi inayoendelea kufanyika Wilayani Muleba.
Akizungumza katika Hafla hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba amesema kuwa wao kama viongozi wanatakiwa kuyatekeleza yote yanayohitaji utekelezaji katika Wilaya ya Muleba kwa lengo la kujenga Wilaya.
" Mafanikio hayaji kwa kufanya kazi kila mmoja kivyake ili muweze kufanikiwa ni lazima msimame nyote kwa pamoja kwahiyo sisi kama Serikali ni jukumu letu kuendelea kusimamia mazingira mazuri ya usalama na amani ili kazi zote zinazofanyika ziwe ni kazi endelevu" amesema Ndg. Greyson Mwengu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba amemuomba Mkurugenzi Mtendaji kusimamia miradi inayotekelezwa ndani ya Wilaya ya Muleba kwa bajeti zinazopangwa pamoja na fedha inayotoka Serikali kuu ili iweze kuwanufaisha wananchi kama inavyostahili.
Lakini pia amesema kuwa kwa Mwaka huu wa fedha tayari Halmashauri imeshatoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.7 kwa ajili ya makundi ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu ili kuweza kuwasaidia kutekeleza miradi yao, kuzalisha na kuboresha maisha yao.
Katika uzinduzi wa Makala ya utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyofanyika kwa kipindi cha Miaka Miwili ya Mhe. Dr Samia Suluhu Hassan wilaya ya Muleba ilipokea jumla ya kiasi cha Tsh. Bilioni 40.5 ambazo zilielekezwa katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Elimu, Afya, Nishati, Kilimo, Uvuvi, Maji na Nyinginezo.
Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa