Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr. Mwigulu L. Nchemba (MB), amezindua zoezi la usajili na utambuzi wa watu Mkoa wa Kagera lengo likiwa ni kuwasajili wananchi na kuwapatia vitambulisho vya Taifa (NIDA), ambapo ki mkoa uzinduzi huu umefanyika Wilaya ya Muleba, Kata Kyebitembe, Kijiji Kasindaga.
Akizindua zoezi hilo, Dr, Mwigulu Nchemba amewasisitiza wananchi kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi kwani kitambulisho hiki ni cha muhimu sana kwa mtanzania.Pia amewahasa kuwa waaminifu na kuhakikisha wanaosajiliwa ni wakazi halali wa eneo hilo.
Amesisitiza juu ya amani ya nchi yetu na kukemea mauaji yanayoendelea katika nchi yetu.Na kumwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina juu ya mauaji yaliyotokea Kinondoni, Jijiji Dar es Salaam
Uzinduzi huu umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Sekretariet ya Mkoa, Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya, Meya/Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, Viongozi wa Vyama na Viongozi wa Dini, Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa