Katika kikao cha Baraza la Madiwani kujadili mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe Toba Nguvila amewahimiza madiwani kwenda kutoa elimu kwa wazazi kuchanga vyakula kwa ajili ya watoto kupata chakula mashuleni.
Akizungumza katika baraza hilo amewaeleza waheshimiwa madiwani kuwa mtoto akipata lishe bora akiwa shuleni udumavu wa akili unaondoka jambo ambalo linachangia katika kuongeza ufauru kwa mtoto kuwa mzuri.
"Chakula cha mchana ni kichocheo chanya kwa watoto kuweza kufanya vizuri kwenye masomo yao kwahiyo ni vizuri madiwani twende na msemo mmoja kwamba ufauru uendane na chakula cha mchana kwa watoto wetu" amesema Mhe. Toba Nguvila.
Akizungumzia suara la michango ya jamii kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu inahitaji vikao kuanzia kwenye eneo hu sika na kuhakikisha kwamba suara hilo linapitishwa katika ngazi zote za uongozi kuanzia kwa Mkurugenzi mpaka kwa mkuu wa wilaya ambapo amewaeleza kuwa Mkuu wa wilaya ndiye anayeidhinisha kutoa kibali cha kuchangisha.
Sambamba na hayo Mkuu wa wilaya amewaomba pia madiwani kwenda kuhamasisha vijana kujihusisha na shughuli za kilimo katika kata zao ambapo amewaomba wahamasishe walau kila kijana awe hekali moja ya shamba ili kuweza kusaidia upatikanaji wa vyakula.
"Hatuwezi kuwa na vijana ambao wanawaza kulishwa tu tutoke sasa tuhamasishe kila kijana awe na hekali moja ya chakula alime mazao avune kwa ajili ya kuwa na hazina ya chakula" Amesema na kusistiza Mhe. Toba Nguvila.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amewaomba madiwani kutochanganya shughuli za Chama na shuguli za kiserikali ambapo amewaeleza kuwa ikijengwa hoja ya madiwani kupatiwa mafuta kuhamasisha vikundi suara hilo litakuwa la kichama zaidi na halitakuwa la kiserikali.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justus ametoa pongezi kwa madiwani kwa kupitisha mpango wa bajeti ya mwaka 2022/2023 na Kumshauri Mkurugenzi pamoja na wataalamu kuhakikisha wanatekeleza miradi yote kupitia bajeti hiyo kwa kuwaeleza kuwa kupitia bajeti hiyo ndio dira ya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Lakini pia Kaimu Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Evart Kagaruki amewaeleza madiwani kuwa Halmashauri haiwezi kujenga katika maeneo ya TANROAD au TARURA kwa kuwaeleza kuwa tayari Halmashauri inaandaa mpango wa kujenga kitegauchumi katika maeneo ya soko la Muleba mjini.
Ameongeza kwa kuwaeleza madiwani kuwa kwa sasa ofisi ya Mkurugenzi inazo posi za kutosha kwa kuwaomba kwenda kuwambia watendaji wenye uhitaji wa posi kwenda kuchukua posi katika ofisi ya mweka hazina kadri ya uhitaji wao.
Baraza limeidhinisha na kupitisha kiasi cha shilingi bilioni 74, 446, 017, 639. 88/= ili ziwe fedha zitakazotumika kutekeleza mpango wa bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa