Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (MST) Salum M. Kijuu amezindua zoezila chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi Mkoa wa Kagera kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka 14, katika kituo cha Afya Kaigara, Kata Muleba, Wilaya yaMuleba.
Akizindua zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa amewasihi watoa huduma wa chanjo yasaratani ya mlango wa kizazi kuhakikisha wanafanikiwa kufikia lengo la kiwilayakama walivyopangiwa na wizara kwani ugonjwa huu umekuwa ukiwatesa sana mabintina akina mama. Na kwa kuwa kinga imepataikana ni vema kuokoa kizazi cha sasakisiangamie kwa ugonjwa huu.
"Kama tunavyofahamu ugonjwa wa saratani hasa kwa akina mama umekuwatishio, japo taifa letu ugonjwa huu haujakuwa kwa kasi kubwa ukilinganisha namataifa mengine, ni vema sasa tukahakikisha kila binti mwenye umri wa miaka 14anapata chanjo hiyo ambayo ni kinga dhidi ya ugonjwa huo. Aidha, chanjo hiyoitatolewa mara mbili yani baada ya miezi sita ili kukamilisha dozi",alieleza Meja Jenerali (MST) Salum Kijuu.
Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa ametoa vyandarua kwa wanafunzi wa shule za msingiikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Malaria Duniani ambayo kilele ni siku ya tarehe25/04/2018. Kauli Mbiu ni "Niko Tayari Kutokomeza Malaria Wewe Je".
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa