Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila amewahimiza wafanyabiashara wa wilaya ya Muleba kuacha kupandisha bei kwa bidhaa zinazopatikana ndani ya maeneo ya wilaya ya Muleba ili kuepuka kuwaumiza wananchi alipokutana na Wafanyabiashara katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba.
Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa wilaya amewasihi wafanyabiashara kuwajali wateja wao ili waweze kupata faida ambayo ni halali bila kuwaumiza wananchi kwa kuwauzia bidhaa kwa bei ya juu.
"Tukizingatia hayo tutakuwa na wateja wengi,watakuja wengi, mtafanya biashara nyingi na mtapata faida kubwa hata upendo kwenye jamii utakuwa mzuri mkiuza bidhaa zenu kwa wananchi kwa bei ambayo ni nzuri"
Aidha, amewaeleza wafanyabiashara kuwa kadri wanavyoagiza mzigo mala kwa mala na kuuza kwa bei nafuu watakuwa kwenye nafasi ya kupata faida zaidi.
Lakini pia Mkuu wa wilaya ameagiza kufanyika kwa Baraza la Wafanyabiashara mala mbili kwa mwaka ili kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu wafanyabiashara pamoja na wanufaika wa biashara, kukuza afya ya biashara na kutatua changamoto mbalimbali za wafanyabiashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amewasihi wafanyabiashara kuacha ubinafsi kwa kuwaeleza kuwa sio jambo jema kupandisha bei ya vitu vilivyomo kwenye maduka yao baada ya bei elekezi kutangazwa na serikali.
Naye Katibu Mkuu wa wilaya ya Muleba Ndg. Gleyson Mwengu amewaomba Wafanyabiashara kuweka bei zenye uafhadhari ambazo haziwaumizi wananchi hasa kwa bidhaa zilizomo ndani ya wilaya kwa kuwaeleza kuwa wakiendelea kupandisha bei hasa ya bidhaa ya vyakula wanaweza kupelekea mlipuko wa magonjwa hata ya utapiamulo kwa wilaya ya Muleba.
Afisa Biashara wa wilaya ya Muleba amewaomba wafanyabiashara kupunguza bei hasa kwa bidhaa kama mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia bidhaa za ofisini kama karatasi nyeupe na vyakula kama nyama vishushwe bei na kuunzwa kwa bei yenye uafadhari.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa