Timu ya Kurugenzi Fc ya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera leo imeanza safari ya kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Shirikisho la michezo ya Serikali za mitaa Tanzania Shimisemita ngazi ya Taifa huku wakitakiwa kushindana kwa bidii ili kuleta ushindi nyumbani.
Akizungumza wakati wa kuwaaga wachezaji wa timu ya kurugenzi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bw. Evart Kagaruki amesema kuwa mashindano hayo yanataanza kesho agosti 25 katika viwanja vya Butimba.
Aidha,Bw. Kagaruki amewataka wachezaji hao kushiriki kwa bidii na nidhamu kwani ndio njia pekee ya mafanikio ya ushindi na hujenga mahusiano mazuri baina ya washiriki.
Naye afisa michezo na utamaduni Wilaya ya Muleba Bw. Denis Joseph amesema kuwa michezo itakayochezwa itajumuisha mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa mikono, mpira wa wavu, riadha, pultebo, mchezo wa karata, drafti na mchezo wa kuvuta kamba.
Nao baadhi ya wachezaji wa Kurugenzi Fc ambao ni Hosea Shedrak, Victa Kaijage na Dawson Mbabazi wameushukuru uongozi wa Halmashauri kwa kuwawezesha kushiriki mashindano hayo na hivyo kuahidi kushiriki kwa bidii ili kuketa ushindi nyumbani.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu: 0744644702
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa