Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justus ameipongeza Timu ya Halmashauri iliyoshiriki katika mashindano hayo kwa kurudi na ushindi na kuifanya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kuwa miongoni mwa Halmshauri zilizoshiriki na kushinda baadhi ya michezo iliyofanyika.
"Lazima kuwepo vikao vya mara kwa mara kutathmini michezo na kupitia Mkuu wa Idara ya Utamaduni niwe napata taarifa za mara kwa mara mkikwama popote nipate taarifa ili kuwezo kuona namna ya kuweza kutatua changamoto yenu" amesema Mhe. Magongo Justus.
Katika Taarifa iliyosomwa na Kapteni wa Timu Ndg. Mosses Kuyyela amesema kuwa katika michezo waliyoshiriki wameweza kushinda kikombe cha mshindi wa tatu kwa kuvuta Kamba Kitaifa (kati ya Halamshauri 110), wameshinda midali ya mshindi wa tatu katika michezo ya riadha mita 400, wamekuwa Halmashuri ya 6 bora kitaifa katika mashindano hayo ( kati ya 110) pamoja na kufanikiwa kuingia 8 bora Kitaifa na michezo mingine kuingia nusu fainali.
Sambamba na hayo ameongeza kwa kuuomba uongozi wa Halmashauri kutoivunja timu iliyoshiriki mashindano ya SHIMISEMITA Dodoma ili timu hiyo iwe pamoja kwa muda wote kwa kuwa na ratiba ya kukutana na kufanya mazoezi ya Pamoja, timu kushiriki katika mashindano mbalimbali yanayojitokeza ili kuijengea uzoefu, kuwa na mechi za kirafiki ndani na nje ya Wilaya lakini pia Ofisi ya Utamaduni kuendelea na zoezi la kutafta wachezaji wengine na kuwaunganisha na timu ili kuongeza nguvu katika timu.
Mashindano haya yamefanyikia katika Jiji la Dodoma kuanzia tar 17-31/10/2023, yakiwa na kauli mbiu ya ‘ IMARISHA AFYA NA MAHUSIANO KAZINI KWA MAENDELEO YA NCHI”. Halmashauri ya wilaya ya Muleba ni moja kati ya Halmashauri 110 zilizoweza kushiriki mashindano haya kwa mwaka huu. Halmashauri iliwakilishwa na wafanyakazi 30 ambapo kati ya hao viongozi walikuwa 3 na wanamichezo 27. Wanamichezo hawa walishiriki katika mashindano hayo katika michezo mbalimbali ikiwa ni Pamoja na Mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa wavu, mpira wa mikono, kuvuta Kamba, karata, bao, pooltable na riadha.
Imetolewa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa