Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila katika kikao cha kujadili mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Narphin Hotel amewasihi TARURA kwamba wanapojenga Barabara waweke njia za mifugo kwani mifugo ikiendelea kupita barabarani barabara zitaharibiwa na mifugo hiyo.
Akizungumza katika Kikao hicho amewambia TARURA kuwa watoke katika mfumo wa kujenga barabara kila mwaka waende sasa kujenga barabara ambazo zitadumu kwa miaka kadhaa ambapo amewashauri kwamba ni bora wakajenga barabara chache kwa kiwango cha moramu kuliko kujenga barabara ambazo hazina Moramu kwa kuwaeleza kwamba kuwa na kilometa nyingi haisaidii kama hizo barabara hazitakuwa kwenye kiwango cha Moramu.
"Ninafuu tujenge barabara chache zidumu kwa mda mrefu kuliko kujenga barabara nyingi za kufanyia marekebisho kila mwaka hatuwezi kusonga tusipogundua hilo tutakuwa tunapoteza fedha nyingi bila kuwa na sababu ya msingi sisi wote ni wataalamu waheshimiwa Madiwani ni wazoefu sana tuone tutoke huko tujenge barabara angalau za kiwango kizuri zitakazodumu kwa mda mrefu"
Aidha mheshimiwa Mkuu wa wilaya ameongeza kwa kusema kuwa Barabara ya Rutolo kutoka Ngenge kwenda mpaka Rutolo pamoja na barabara ya Mziro kwenda mpaka Burigi zimewekwa kwenye mpango maalumu ambapo amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa Barabara hizo zikikamilika ziitawasaidia wananchi wa maeneo hayo kwenye usalama wa eneo na huduma kwa wananchi.
Lakini pia ametoa pongezi kwa walimu kuwafaurisha wanafunzi katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2021 yaliyotoka hivi karibuni ambapo ameendelea kuwasisitiza walimu kuongeza kasi ya ufundishaji ili wanafunzi waweze kufauru zaidi.
"Tulishakubarina Mhe. Mwenyekiti kwenye vikao vya Baraza walimu wanaofanya vizuri vile viwanja vyetu tisa vitengwe kwa ajili ya kuwapa zawadi walimu waliofanya vizuri kwa kufaurisha wanafunzi katika masomo yao"
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Muleba Eng. Dativa Thelesphory katika kikao hicho cha kujadili mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ameleeleza kuwa TARURA wamepanga kutumia bajeti yenye ukomo wa Tsh. bilioni 4, 380, 307, 726.00 katika matengenezo ya barabara mbalimbali kutoka vyanzo vitatu vya fedha ambavyo ni Mfuko wa Barabara, Mfuko wa Jimbo na Tozo za mafuta.
Naye Kaimu afisa Mipango Ndg. Evart Kagaruki ameeleza kuwa Makisio kwa Mwaka 2022/2023 Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya wilaya inakadilia kukusanya jumla ya Tsh. 74, 446, 017, 639.88 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo ni pamoja na Mapato ya ndani, Ruzuku za - Mishahara, Ruzuku za Miradi pamoja na Ruzuku za OC.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa