Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Joyce Ndalichako, ametembelea na kukagua shughuli za elimu wilyani Muleba ikiwa ni majengo na taaluma za shule .Ziara yake ilianzia Chuo cha Ualimu Katoke ambapo amepokelewa na Uongozi wa Wilaya na kusomewa taarifa ya wilaya kisha kutembelea majengo ya chuo hicho.
Baada ya hapo alielekea shule ya Sekondari Prof.Joyce Ndalichako iliyopo kata Rulanda na kulakiwa na wananchi. Alikagua majengo ya shule na kuhutubia, ambapo amewapongeza wananchi,uongozi kata na wilaya kwa kusimamia ipasavyo ujenzi wa shule hiyo kwani ni viwango. Amehaidi kuongeza Tshs 50,000,000.00 kwa ajili ya kuongezea nguvu ya wananchi katika ujenzi wa maabara na Tshs 3,00,000.00 kwa ajili ya ununuzi wa vitabu.
Pia ameahidi kutatua tatizo la ukosefu wa maji kwa kuagiza Uongozi wa Wilaya kutafuta mtafiti atakayeweza kubaini upatikanaji wa kisima cha maji. Mwisho amemalizia ziara yake shule ya sekondari Anna Tibaijuka na kuahidi mabati 100 na ufungaji wa umeme.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa