Ikiwa leo tarehe 08 Januari,2024 Shule zote za Sekondari na Msingi zinafunguliwa kote Nchini, Kamati ya Usalama(KU) inayoongozwa na Mhe.Dkt.Abel Nyamahanga kwakushirikiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bi.Christina Akyoo pamoja na baadhi ya wataalamu(CMT)wamefanya uzinduzi wa Shule mpya ya Sekondari Kasheno iliyopo katika kijiji cha Kasheno kata ya Magata Karutanga Wilaya ya Muleba.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shule hiyo Mhe.Dkt.Abel amesema kuwa zaidi ya Wanafunzi 18,105 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza katika Shule za Sekondari zilizopo Wilaya ya Muleba,Wavulana wakiwa 8,738 na Wasichana 9,367 na huku kati yao Wanafunzi 148 wakiwa wamechaguliwa kujiunga na Shule Mpya ya Sekondari Kasheno ambayo itakuwa na Wavulana 75 na Wasichana 73.
Aidha,Mhe.Dkt.Abel amewasisitiza na kuwaonya wazazi wote ambao watawazuiza Watoto wao kwenda Shule nakusema kuwa Mzazi au Mlezi atakae mzuia mtoto wake Kwenda shule hatua Kali zitachukuliwa Ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashtaka.
"Tutakwenda nyumba kwa nyumba,kitanda kwa kitanda kuhakikisha tunakamata wale wote ambao hawajatekeleza agizo la Serikali na tamko hili nila Wilaya nzima hivyo wazazi msiijaribu Serikali".
Pamoja na hilo pia Mhe.Dkt.Abel ametumia muda huo Kumshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwakutoa fedha nyingi za Miradi ya Elimu katika Wilaya ya Muleba ambayo itakwenda kuweka kumbukumbu na alama kubwa kwa Vizazi Vijavyo katika Wilaya ya Muleba.
"Naungana na Wenzangu wote Kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Samia Suluhu Hassani kwa hiki alichotufanyia wana Muleba, jambo ambalo haliwezi kusahaulika hivyo na sisi Wazazi nimashahidi kwani Watoto wetu walikuwa wakitoka Umbali mrefu kwenda kupata Elimu."
Kwa upande wake nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi.Christina Akyoo amesema kuwa ofisi ya Mkurugenzi kwa Kushirikiana na Walimu kwa pamoja watahakikisha majengo yote ya Shule yanakuwa safi muda wote.
Imeandaliwa na kutolewa na;
Eusebius J.Kiluwa
KAIMU MKUU KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa