Katika ziara iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila wilayani Muleba amekagua ujenzi wa barabara inayofahamika kwa jina la barabara ya Shughuli za Usalama na kuwaagiza TARURA Muleba kuhakikisha kazi za ujenzi wa Barabara zinazingatia ubora unaostahili.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ni vema barabara ikajengwa kwa kuzingatia ubora unaostahili ili kuepusha changamoto za barabara kuhalibika ndani ya kipindi cha mda mfupi.
"Kazi ikiwa bora maana yake ni kwamba mmelinda rasilimali fedha lakini pia inakuwa imewaepusha na ninyi wenyewe kuhisiwa kwamba ni wala rushwa kwa sababu kazi isipokuwa nzuri na mtaalamu ukawa umeiona na haujasema chochote maana yake ni kwamba Rushwa kama adui wa haki anakuwa ashapita maofisini kwenu" amesema Mhe. Albert Chalamila.
Lakini pia amewahimiza ofisi ya TARURA kuhakisha wanasimamia ujenzi wa barabara hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati.
Katika Taarifa iliyosomwa na Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Muleba Eng. Pius Malegesi amesema kuwa ofisi ya TARURA iliidhinishiwa kiasi cha Tsh. Milioni 400 kwa mwaka wa fedha 2022-2023 kujenga barabara inayoitwa Shughuli za Usalama yenye ulefu wa mita 700 kwa kiwango cha lami na itagharimu kiasi cha Tsh. Milioni 399.9,bila ongezeko la thamani.
Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa