Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila amefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na kuiagiza ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilayani Muleba kuwa na utaratibu wa kuandaa makala za utekelezaji wa miradi toka inapoanza mpaka kukamilika.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali hiyo Mkuu wa Mkoa amesema kuwa uandaaji wa makala za miradi toka inapoanza kutekelezwa mpaka kukamilika itasaidia kuweza kudhibitisha hali halisi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
"Mkiandaa makala za utekelezaji wa miradi itaweza kuwasaidia kueleza kwa nini fedha hazijatosha endapo mradi usipokamilika kwa sababu fedha inaweza ikaletwa maeneo yote kiwango kile kile lakini isitoshe kutokana na eneo lilivyo sasa ukiwaonesha kwa makala tangu unachimba msingi itakisaida kupunguza maswali kwa nini fedha haikutosha kukamilisha mradi huo" amesema Mhe. Albert Chalamila.
Lakini pia amewasihi kuhakisha wanawatumia wadhabuni wanaonunua vifaa vilivyo bora na vinavyokidhi viwango vilivyowekwa na wahandisi wa ujenzi ili kuweza kuondoa changamoto ya kuuziwa vifaa visivyo bora.
Katika taarifa iliyosomwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dr. Deo Kisaka amesema kuwa Halmashauri ilipokea kiasi cha Tsh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya awali ya Hospitali ya Wilaya ambapo limejengwa jengo la Wagonjwa wa nje na jengo la Maabara na mpaka sasa ujenzi wa mradi huo kiasi cha Tsh. milioni 493.5 kwa ajili ya kuwalipa wadhabuni wa vifaa vya ujenzi vya viwandani na vifaa vya asili pamoja na mafundi wa ujenzi na kiasi kilichobaki mpaka sasa ni Tsh. milioni 6.4 na kiasi hicho kipo kwenye mchakato wa malipo ya mafundi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu: 0769106793
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa