Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dr Abel Nyamahanga kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi anayetekeleza mradi wa Maji Kyamyorwa ili uweze kukamilika kwa viwango vinavyostahili.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ni mambo mengi ambayo mkandarasi anapaswa kusimamiwa ikiwa ni pamoja na kuzingatia ubora wa simenti pamoja na nondo anazozitumia katika ujenzi wa mradi.
"Inaweza ikatokea maji haya yakawa mengi sana hivyo inatakiwa uimara na ubora wa ule ukingo ili mwisho wa siku maji yasije yakabomoa ukuta wa ukingo huu" amesema Mhe.Albert Chalamila.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dr Abel Nyamahanga amemhaidi Mkuu wa Mkoa kuwa watahakikisha wanamsimamia Mkandarasi huyo ili aweze kukamirisha mradi huo kwa viwango vinavyostahili kama alivyoagiza.
Diwani wa Kata ya Kasharunga Mhe. Theobadi Kulandebe amemuomba Mkuu wa Mkoa kuchimbwa kwa visima virefu vya maji kwa vitongoji ambavyo havitafikiwa na huduma ya mradi huo.
Katika Taarifa iliyosomwa na Eng. Kaiza Zefulini kaimu Meneja Rowasa Muleba amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za benki ya Dunia chini ya programu ya lipa kwa matokeo ijulikanayo kama (PforR) mpaka kukamila mradi utagharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 3.7
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa