Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu imefanya ufadhiri kwa vikundi viwili vya vijana kwa kutoa mashine za kukata vioo pamoja na vyerehani kwa kikundi cha Vijana Bujuna na kikundi cha Tujenge Chetu vilivyopo wilayani Muleba kama sehemu ya kuviwezesha vikundi hivyo.
Akizunguza wakati akikabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justus amewasihi vijana hao kuvitunza vizuri vifaa hivyo ili viweze kutumika kwa mda mrefu katika kazi zao kwa ajili ya kuwanufaisha zaidi.
"Wapo watu ambao sio wazuri sana katika kutunza vifaa au mali ambayo amepata bila kutoka jasho lakini mjue kwamba hii mmeshaitolea jasho mlipopokea mkopo mkaendelea kuzarisha ndipo kazi yenu ikaonekana kutokana na kazi manazozifanya kwahiyo niwatie moyo muendelee kufanya kazi vizuri ili muweze kupata manufaa zaidi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndg. Stewart Mtondwa ameeleza kuwa vifaa hivyo vimetolewa kwa vikundi hivyo ikiwa pia kama ishara ya kuonesha ni kwa jinsi gani Halmashauri inachangia asilimia 10 za mapato ya ndani kwa kutoa mikopo kwa vijana ambapo vilichukuliwa vikundi vinne Mkoani ambavyo vinafanya vizuri na Mkoani wakapeleka Wizarani ndipo Wizara ikaamua kufadhiri vikundi hivyo.
Kwa upande wake Bw. Kervin Alistides Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana Bujuna ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu kwa kuwapatia vifaa hivyo ambapo ameeleza kuwa kupitia vifaa hivyo vitaweza kuwasaidia kufanya kazi za wateja kwa wakati na kuwaondolea changamoto yakutomaliza kwa wakati kazi za wateja kutokana na kutumia vifaa vya kukodi walivyokuwa wanavituia awali.
Naye Bi. Alodia Mwijage amesema kuwa hapo awali walikuwa wanapata changamoto yakutokidhi mahitaji yao kutokana na uhaba wa cherehani lakini kupitia vyerehani walivyopewa wanaaamini wataweza kufanya kazi zao vizuri na wataweza kuwahamasisha na vijana wengine kuunda vikundi kama wao.
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye imetoa ufadhiri wa Mashine Mbili za Kukatia vioo na mashine mbili za kutobolea vyuma na mbao zenye thamani ya Tsh. Milioni 3.3 na pamoja na Vyerehani vitatu vyenye thamani ya Kiasi cha Tsh. Milioni 2.6 kwa kikundi cha Vijana Bujuna kilichopo Kata ya Izigo na Kikundi cha Tujenge Chetu kilichopo Kata ya Mayondwe.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa