Katika Mkutano wa hadhara uliofanywa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Albert Chalamila ameiagiza ofisi ya Mkurugenzi kuwataftia eneo litakalowafaa Wafanyabiashara wa soko la Kariakoo lilopo katika Muleba mjini katika kipindi cha ukarabati wa soko hilo.
Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa ameagiza pia zoezi la ukarabati wa soko hilo kufanyika kwa wakati na kukamilika haraka ili wananchi waweze kurudi katika soko hilo na kuendelea na biashara zao kama ilivyokuwa awali.
"Kama mnahisi kuna jambo gumu bado lipo kuhusu kuhama na kupisha eneo la Soko kwa ajili ya ukarabati rudini tena kwenye vikao mkae tena na kuona ni kwa namna gani litatafutwa eneo ambalo litafaa kwa ajili ya kufanya biashara zenu" amesema Mhe. Albert Chalamila.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justu ameeleza kuwa baada ya uchakavu wa miundombinu ya soko la Kariakoo ambalo linamilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Muleba na kilitengwa kiasi cha Tsh. milioni 145 kwa ajili ya ukarabati wa soko.
Lakini pia ameongeza kwa kusema kuwa kwa awamu ya pili itabadirishwa sura ya mbele ya soko hilo ambalo litajengwa kwa mwonekano wa ghorofa ambapo Halmashauri imetenga kaisi cha Tsh. milioni 350 na eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya wafanyabiashara ni eneo la Omkalyambwa ambapo tayari vyoo vimejengwa na TANESCO wako kwenye mpango wa kupeleka umeme katika eneo hilo.
Sambamba na hayo Mwenyekiti wa Halmashauri amesema kuwa watakaa na wafanyabiashara na kujadiliana kwa pamoja kuona ni kwa namna gani watakaa sehemu salama ya kufanyia biashara zao wakati ukarabati wa soko hilo utakapokuwa ukifanyika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amesema kuwa bado ukarabati wa soko hilo haujaanza bali watakaa nao kujadiliana lakini sio kwamba ndo wametolewa katika eneo hilo.
Naye Diwani wa Kata ya Muleba Mhe. Muhaji Bushako ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba amewaeleza wafanyabiashara kuwa wote watapangwa katika eneo ambalo limepangwa na watawadhibiti wote watakaoekwenda mitaani kuwaharibia biashara yao.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa