Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dr Abel Nyamahanga ameiagiza Ofisi ya Ardhi kuhakikisha ifikapo tarehe 12 /04/2023 vieelezo vyote ikiwa ni pamoja na Ramani inayotenganisha Kijiji Kasheno na Kijiji Magata viwe vimeshapatikana ili kuweza kutatua mgogoro wa Ardhi uliopo kati ya Kijiji Bureza Kata ya Bureza na Kijiji Kasheno Kata ya Magata Wilayani Muleba.
Akizungumza alipofika katika eneo hilo Mkuu wa Wilaya amewaeleza Wananchi wa Vijiji hivyo kuwa migogoro ya ardhi inakwamisha shughuli za maendeleo na inaweza kusababisha kuvunja amani na kuhatafisha maisha ya watu hivyo ni vema Ramani ikatumika ili kiweza kubainisha mipaka sahihi ya vijiji hivyo.
"Niwaombe sana tuendelee kuwa wavumilivu tuendelee kulinda amani na tuendelee kiwa watulivu mpaka ramani itakapo fika na ni mwiko wananchi kujichukulia sheria mkononi niwaombe sana wanachi mfuate maelekezo hayo mpaka tutakapokuja kumaliza mgogoro huu
Lakini amewasihi wananchi kutofanya shughuli yeyote katika eneo zikiwemo shughuli za kilimo mpaka mgogoro utakapokuwa umetatuliwa na kumalizika.
Kwa upande wake Afisa Ardhi Ndg. Saimon Mosha ameeleza kuwa tayari ameshaandika barua kwa Kamishina wa Ardhi kumuomba msoma ramani kufika eneo hilo ili kuweza kuwanyesha mipaka sahihi ya eneo hilo na amehaidi kuhakikisha anafuatilia na kupata ramani sahihi inayotenganisha vijiji hivyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mahusiano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa