Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila amewasihi ofisi ya TARURA Wilaya ya Muleba kuhakikisha wanafanya manunuzi ya vifaa kwa kufuata vigezo vinanvyostahili ili kuweza kuepuka changamoto ya kuuziwa vifaa visivyo na ubora.
Akizungumza wakati wa Ukaguzi wa Taa zilizowekwa katika barabara za Mitaa Muleba Mjini Mkuu wa Mkoa amewasisitiza TARURA kuhakikisha wanawatumia wadhabuni wanaonunua vifaa vinavyokidhi viwango vya ubora ili kudhibiti kunuliwa kwa vifaa visivyo na ubora.
"Zidisheni vigezo vya ubora zaidi katika manunuzi ya vifaa vyenu ili muweze kudhibiti ununuzi wa vifaa visivyo bora na hivi vigezo lazima viandikwe na ninyi watu wa TARURA kuhusiana na ubora wa vifaa mnavyovihitaji msipofanya hivyo makampuni ni mengi yapo yenye ubora na yasiyo na ubora"
Lakini pia amewasihi wananchi Wilayani Muleba kuzitumia taa hizo kufanya biashara masaa 24 kwa kuwaeleza kuwa taa hizo zinapofungwa zinasaidia kuzuia vitendo vya uhalifu lakini zaidi zinasaidia kufungua mji hivyo ni vema wakazitumia taa hizo kuwanufaisha kiuchumi.
Kwa upande wake Kaimu Meneja TARURA Muleba Eng. Pius Malegesi amesema kuwa taa zilizofungwa na Mkandalasi ni taa ambazo zimefata vigezo walivyoviweka TARURA kwa hiyo mwanga unaolalamikiwa na wananchi kuwa hafifu ni kutokana na suala la umbali wa kutoka taa moja kuifikia taa nyingine hivyo kwa mwaka wa fedha unaofuta wataongeza taa katika maeneo yaliyobaki wazi ili taa ziweze kukutana na kuzalisha mwanga ulio mkubwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa