Benki ya NMB ni miongoni mwa wadau wa maendeleo ambao wamekuwa wakishirikiana na jamii na wakiunga mkono juhudi za maendeleo kwa kutoa mahitaji mbalimbali hususani sekta ya Elimu. Ambapo wamekabidhi vitanda 80 na magodoro 160 yenye thamani ya Tsh. 27.6 kwa Halmashauri ya Wilya ya Muleba kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi Kaigara.
Akiwapongeza wakati wa hafla ya kukabidhi vitanda 80 (double decker) na magodoro 160, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Magongo Justus ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, iliyofanyika shule ya msingi Kaigara, ameishukuru benki ya NMB kwakuwa mdau mkubwa wa kuchangia shughuli maendeleo na kuwasihi kutochoka kujitoa kwa ajili ya jamii kwani bado kuna uhitaji mkubwa.
“Ninayo furaha kubwa sana asubuhi ya leo kuwa mgeni rasmi nyumbani, ambapo tunapokea ufadhili mkubwa sana kutoka benki ya NMB, nianze kwa kusema neno sana asanteni. Uwepo wa kituo hiki si kwa bahati mbaya ni kwasababu Serikali inatambua uhai na ustawi wa kila mtu, kumekuwepo baadhi ya tabia ya wazazi akishajaliwa zawadi ya mtoto ambae anamahitaji maalum asilimia kubwa wamekuwa wakiwaficha watoto hao. Serikali kwa kugundua hilo kukawepo sera na miongozo ya kuhakikisha watoto hawa wana haki ya kupata elimu, kuishi na kuwajali”, ameeleza Mhe. Magongo
Aidha, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaweka mipango thabiti ya kuhakikisha inamfikia kila mmoja na kwa mahitaji yake. Hivyo tukio hili litufanye kuwa mabalozi popote pale tunapojua kuna watoto wenye uhitaji maalum na wamefichwa ndani tuwabaini na kuhakikisha wanaletwa katika vituo/shule zinazotoa elimu kwa watoto hawa.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda wa NMB, Ndg. Baraka Ladislaus kwa ameipongeza Serikali kwa kuboresha sekta ya elimu ikiwemo miundombinu ya kujifunzia na elimu bure ambapo Serikali imeongeza wigo wa kuwalipia wanafunzi wa kidato cha tano na sita ada ya masomo. Na wao kama wadau wanao wajibu wa kuunga juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali, kwa kuisaidia jamii kwani jamii ndio imeifanya benki hiyo kuwa kubwa kuliko benki zote Tanzania.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa