Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila amewaomba wadau wa Kahawa kutoa ushirikiano kupambana na kukomesha utoroshaji wa kahawa kwa njia ya magendo.
Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa wilaya ameielekeza kamati ya usalama na pamoja na viongozi wa kata na vijiji AMCOS kuhakikisha wadhibiti magendo kutoka ndani ya wilaya kwenda nje ya nchi bila kufuata utaratibu wa kiserikali uliowekwa.
"Jukumu la kwanza la kwetu sote ni kuhakikisha tunaweka utaratibu mzuri wa kuzuia na kuepusha biashara ya magendo ya kahawa" amesema Mhe. Toba Nguvila.
Aidha, Mkuu wa wilaya amewaomba viongozi wakiwemo watendaji, maafisa kilimo pamoja na Amcos kuhakikisha wanatoa elimu kupambana kuhakikisha wanazuia baishara ya kuuzia kahawa mashambani ili wananchi wote wenye kahawa waweze kuuza kahawa yao kwenye mnada.
Lakini pia amewaomba wakulima wa kahawa kuhakikisha wanatunza kahawa vizuri ili thamani ya kahawa yao iweze kupanda ambapo amewasistiza kuwa wakitunza kahawa yao vibaya thamani yake itashuka hivyo ni vyema wakahifadhi kahawa zao kwenye maghara bora.
Sambamba na hayo amewaomba wafanyabiashara kuhakikisha wanafuata mwongozo uliotolewa ambapo amewasihi kuwa kwa mfanyabiashara atakayekiuka masharti hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Imeandaliwa na Kutolewa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa