Katika zoezi la kupambana na uvuvi Haramu Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila pamoja na Kamati ya Usalama wamefanya oparesheni ya kuchoma dhana za uvuvi haramu Katika kata saba wilayani Muleba zenye dhamani ya Tsh. Milioni 137.3.
Akizungumza katika zoezi hilo Mkuu wa wilaya amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa ili kuweza kuwabaini na kuwakamata wale ambao hawajasalimisha dhana haramu ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
"Tumejipanga kutokomeza uvuvi haramu tumejipanga kuendeleza uvuvi endelevu uvuvi haramu ni lazima tuupinge, uvuvi haramu ni lazima tuukatae kwa faida za kizazi hiki tusipofanya hivi hali itakuwa mbaya afya zitakuwa mbaya vijana wetu watakosa lishe, hata masoko ya samaki hayatakuwa na faida" amesema Mhe Toba Nguvila.
Aidha, Amesistiza mitumbwi yote kutia nanga kwenye maeneo ya BMU na hata wanapokwenda kuvua lazima mitumbwi yote itoke kwenye maeneo ya BMU na kama kuna mitumbwi haijasajiliwa ni lazima isajiliwe kwa kusema kuwa mitumbwi ambayo haijasajiliwa ndio mabingwa wa uvuvi haramu.
Katika zoezi hilo amemsimamisha Mwenyekiti wa BMU Mwalo wa Nyakigera, Kijiji Kiziramuyaga, Kata ya Magarini Ndg. Charles Magadula baada ya kubainika kuwa miongoni mwa watu wanaomiliki dhana haramu za kuvulia samaki katika kata hiyo.
Kwa upande wake Afisa Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Ndg. Donatus Dominick amewaomba wananchi kwa kushirikiana na viongozi wasaidie kuunga mkono kutokomeza uvuvi haramu ili kumaliza suara la uvuvi haramu kwenye ziwa Victoria.
Naye Kaimu Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba. Ignasio Rwina amewaomba wananchi pamoja na wadau wa uvuvi kutoa ushirikiano kwa kumuunga Mkono Mkuu wa wilaya pamoja na kamati yake ya usalama ili kuhakikisha uvuvi haramu unakomeshwa katika wilaya ya Muleba.
Sayakulu Suleiman Ismail ameomba viongozi waendelee kudhibiti uvuvi haramu na kwa wale wanaojihusisaha na uvuvi halamu tutoe ushirikiano ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Humaru Amos Rwaikondo Mkazi wa kijiji Misikilo Kata Gwanseli ameeleza kuwa kwa wale ambao bado wamebaki na dhana haramu ni vema wasalimishe dhana hizo haraka kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao na kuhaidi kutoa ushirikiano kuwabaini ambao bado watakuwa wameficha nyavu zao haramu.
Zeozi hilo la uteketezaji wa Nyavu haramu ambazo zimesalimishwa na wwnanchi limefanyika katika kata saba ambazo ni Kata ya Kata ya Kimwani, Kata ya Nyakabango, Kata ya Rulanda, Kata ya Gwanseli, Kata ya Izigo, Kata ya Katoke pamoja na Kata ya Mayondwe na Kuteketeza dhana zenye dhamani ya Tsh. Milioni 137.3.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa