Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile (MB) ametembelea na kukagua shughuli za ujenzi na ukarabati wa vituo vya Afya Kaigara na Kimeya. Ambapo, Kituo cha Afya Kimeya kilipokea kiasi cha Tsh. 400,000,000,000.00 kutoka Ofisi ya Rais- Tamisemi kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho.
Katika ziara yake amewasisitiza wauguzi kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao ili kuleta tija kwa jamii wanayoihudumia.
"Nimefurahishwa na utendaji kazi na majibu ya wananchi juu ya hudumu mnazotoa hususani upatikanaji wa dawa, hivyo nawasihi muendelee kutoa huduma bora za kuwahudumia wananchi hawa," alieleza Dkt Ndungulile
Majengo yanayotarajiwa kujengwa katika kituo cha Afya Kimeya ni pamoja na Jengo la Upasuaji, Maabara, Jengo la wodi ya wazazi, Jengo la kuhifadhi maiti, Kichomea taka na Nyumba ya Mtumishi. Pia katika ziara yake ametembelea Bohari ya Madawa (MSD) iliyopo eneo la Malahala ili kujionea shughuli zinazofanyika na kujiridhisha na ukubwa wa eneo baada ya ombi la Mhe. Profesa Anna Tibaijuka, Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini la kutohamisha Bohari ya Madawa kutoka Wilaya ya Muleba na kuipeleka Wilaya ya Bukoba Vijiji.
Akizungumza na wananchi, Dkt Faustine Ndugulile amewasisitiza wananchi kujiunga na mfuko wa Afya wa Jamii (Bima ya Aya) ili ziwasaidie kutibiwa kwa gharama nafuu hasa wanapougua na kukosa fedha ya matibabu. Amesisitiza juu ya suala la upatikanaji wa madawa wakati wote ili kuwaondolea usumbufu wagonjwa wanapokuja kupata huduma za Afya na kueleza kuwa, kwasasa tatizo la dawa limekwisha kwani Serikali imepandisha bajeti ya Madawa kutoka Tsh. Bilioni 30, mwaka 2015 hadi Tsh. Bilioni 270 kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa