Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justus ametoa pongezi kwa kamati za shule ambazo zimekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na kusisitiza kwa shule ambazo hazijakamikisha, kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa vyumba hivyo kwa wakati.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba hivyo, amewasisitiza walimu kuendelea kujituma na kuhakikisha wanasimamia vizuri ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa kwa umakini. Pamoja na kuwasisitiza Madiwani kuendelea kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi katika mikutano ya Kata na Vijiji kujitoa katika uchangiaji wa shughuli za maendeleo
"Sio kwamba uchangiaji wa shughuli za maendeleo umeisha, ni vema tukaendelea kujitoa katika uchangiaji wa shughuli za maendeleo maana sio madarasa tu bado tuna na upungufu wa vyoo na maboma ambayo yanatakiwa yakamilke ili kuondoa uhaba wa miundombinu katika Wilaya yetu", amesema Mhe. Magongo
Aidha, ameshauri kuanzishwa kwa utaratibu wa kuvuna maji ya mvua kwa kujenga matenki katika ili maji hayo yaweze kusaidia katika shughuli mbalimbali zinazofanyika shuleni.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila ameshauri walimu kufanya mpango wa kuweka mbao kwenye kuta ambazo zinaweza kutumika kama vizuizi vya kulinda kuta ili kuepusha kuta kuharibiwa na viti vya wanafunzi wanaokaa karibia na kuta
Naye Diwani wa Kata ya Ikondo Mhe. Venanti Mugolozi ametoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kutoa kiasi cha Tsh. Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kamishango jambo ambalo litasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo
Shule zilizotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na shule ya Sekondari Bureza vyumba vitatu vya madarasa,shule ya Sekondari Bujumba vyumba sita vya madarasa,shule ya Sekondari Bulembo vyumba viwili vya madarasa,shule ya Sekondari Ruhanga vyumba vitatu vya madarasa,shule ya Sekondari Rukindo vyumba vinne vya madarasa,shule ya Sekondari Rulama vyumba sita vya madarasa,shule ya Sekondari Kishuro vyumba vitatu vya madarasa,shule ya Sekondari Nshamba vyumba vinne vya madarasa na shule ya Sekondari Kamishango.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa