Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Mh. Justus Magongo amekutana na watendaji wa Kata na Vijiji katika kikao kazi maalumu kilichoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwakumbusha juu ya wajibu wao na kusikiliza changamoto zao za kiutendaji.
Akizungumza katika kikao hicho Mh. Justus Magongo amewaomba watendaji wa kata pamoja na vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kutekeleza majukumu yao huku akiwataka kuonesha mabadiliko katika utendaji wao wa kazi na kusisitiza kuchukua hatua kwa watendaji watakaoshindwa kutimiza majukumu yao.
"Tunahitaji kubadilika kwa spidi na tunasisitiza kuwa tutachukua hatua kali kwa watendaji watakaoshindwa kutimiza majukumu yao na tunasema haya tukiwa na nia kwamba watu waweze kujitambua na kutimiza malengo yao ipasavyo" amesisitiza Mh. Magongo.
Aidha, Mh. Magongo ameongeza kwa kusema kuwa nia na madhumuni ni Halmashauri ni ya Wilaya ya Muleba kuwa Halmashauri ya mfano kwa Halmashauri nyingine za mkoa wa Kagera na Tanzania na jambo hili litawezekana kwa kuongeza juhudi zaidi na zaidi ili kufikia malengo yaliyowekwa ikiwemo ukusanyaji wa mapato.
Akizungumzia suala la watendaji kuwa na vikao vya kisheria amewambia watendaji kuwa wao ndo wanatakiwa kuwa vichochezi kwa wenyekiti wa vitongoji na vijiji kwenda kwa madiwani kuwambia suala la kuwa na vikao vya kisheria ili kupitisha na baada ya kupitisha watendaji wawe na jukumu la kuwaalika wananchi waweze kuhudhulia kwenye vikao hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Muleba Mh. Elias Kayandabila amewaomba watendaji wote kutimiza majukumu yao ipasavyo na kusisitiza kuwa ni marufuku kwa mtendaji yeyote aliyepo ndani ya wilaya ya Muleba kuondoka katika kituo cha kazi bila ruhusa na kuwataka watendaji kuridhika na mishahara yao
"Kuanzia sasa ni marufuku kwa mtumishi yeyote aliyeko ndani ya Muleba kuondoka kwenye kituo chake cha kazi bila kufuata taratibu za kisheria huwezi kuwa Mtendaji wa kata halafu anakuja mgeni anakuta mtendaji haupo kwenye eneo lake la kazi na hajaomba ruhusa ya kutokuwepo kwenye eneo la kazi," amesisitiza Bw. Elias Kayandabila.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri na kuhudhuriwa na wakuu wa idara.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa