Katika ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali iliyofanywa na Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango kukagua ujenzi wa shule mpya ya Mshabago iliyopo katika kata ya Mushabago kijiji cha Kyanshenge Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Magongo Justus amewaasa wakazi wa kijiji hicho kuwapeleka watoto wao shule ili wapate elimu bora.
Akizungumza na wananchi wa Mushabago Mhe. Mwenyekiti amewasisitiza wananchi kuwa nafasi za kazi zote zinazotokea wanaopewa kipaumbele ni wenye elimu hivyo watumie nafasi waliyo nayo kuwapeleka watoto wao shule.
"Tuwasomeshe watoto habari ya kubebwa haipo na usiombe mtoto wako abaki kufagia isipokuwa muarobaini ni watoto waende shule wafauru na ndio maana tunaweka mazingira mazuri ili waweze kujitegemea na kuajiliwa Mtu yeyote ambaye amesoma na akatumia mda wake vizuri hakwami "amesema Mhe. Magongo Justus.
Lakini pia amewasisitiza wananchi kuwafundisha watoto wao ujuzi wa maisha ikiwa ni pamoja na kujifunza kazi mbalimbali kama ujasiriamali na shughuli nyinginezo.
Mhe. Mwenyekiti amehimiza wananchi wa kata ya Mushabago kijiji Kyanshenge kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule ili wawwze kupata elimu itakayowasaidia kwwnye maisha yao .
Sambamba na hayo wajumbe wa Kamati hiyo wameshauri kuanza kufanyika mpango wa kuunganisha umeme katika shule hiyo ili kuondoa changamoto ya umeme katika majengo yanayotegemea umeme hasa majengo ya TEHAMA pamoja na maabara.
Katika taarifa iliyosomwa na mwalimu Mkuu wa Shule ya Nyakatanga Mwl. Benetison Mpanju amesema kuwa mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Mushabago unafadhiliwa na Serikali chini ya mpango wa SEQUIP ulitengewa kiasi cha Tsh. Milioni 470, 000, 000 ambapo ujenzi unahusisha majengo ya Utawala, Vyumba nane vya Madarasa, Maktaba, Maabara tatu za Fizikia Kemia na Baiolojia. Jengo la Tehama na Matundu 20 ya vyoo.
Lakini pia Kamati imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la dharula katika kituo cha afya Kaigara na kupongeza kwa hatua ya ujenzi waliyoifia ambapo Mwwnyekiti pia amewaisitiza kuwa wanaaambatanisha na nakala za benki kwenye taarifa zao.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kaigara katika Taarifa ya ujenzi wa jengo hilo amewaeleza wajumbe kuwa walipokea kiasi cha shilingi milioni 300, 000, 000 kwa ajiri ya utekelezaji wa ujenzi wa jengo la dharula ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia hatua ya renta na kiasi cha pesa ambacho kimeshatumika ni shilingi milioni arobaini na tatu laki tatu na elfu arobaini na mbili na mia tano (43, 342,500/=).
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa