Katika zoezi la utiaji saini wa mikataba ya wakusanya mapato wa madereva lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Magongo Justus amewasihi waliosaini mikataba hiyo kufanya kazi kwa nidhamu, juhudi, weledi na utu ili waweze kufanya kazi yao kwa ufanisi.
Akizungumza katika zoezi hilo Mwenyekiti wa Halmashauri amewaeleza kuwa kazi hizo zinahitaji jitihada binafsi ambapo amewambia kuwa kama hawatakuwa na bidii maana yake kazi yao hawataweza kuifanya kwa ufanisi na wakishindwa kufanya kwa ufanisi basi watasimamishwa kazi hizo.
Sambamba na hayo Mwenyekiti amewaomba wakusanya mapato kuwaheshimu watu wote watakao kutana nao kwenye vituo vyao vya kazi kwa kuwambia kuwa umoja wao wa kuwaheshimu watu ndipo Halmashauri itasimama na kila mtu akajisikia vizuri kuishi katika Halmashauri ya wilaya ya Muleba.
"Unapokuwa na Heshima inakubeba na ikikubeba itakufikisha unako kwenda kwa kuheshimu kazi yako heshimu na aliyekusimamia ili kazi iwe ya manufaa na mafanikio makubwa kwako" amesema Mhe. Magongo Justus.
Lakini pia amewasihi waliosaini mikataba ya ukusanyaji wa mapato kuepuka tamaa za kutaka kutorosha mapato kwa kuwaeleza kuwa wakifanya hivo watakuwa wanazitia hatarini kazi zao na hiyo inaweza kuwapelekea kuchukuliwa hatua na kusimamishwa kazi zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amewasihi wakusanya mapato kwenda kutenda haki ili kinachotakiwa kupatikana kwa ajili ya Halmashauri kiweze kupatikana.
Na ameongeza kwa kuwaeleza kuwa umewekwa mda wa matazamio wa miezi mitatu ili kubaini kama kweli mtu ni mtiifu na atakayofundishwa na tabia zake vinaendana kwa kuwambia kuwa ndani ya miezi mitatu wataweza kuona kama mtu anafaa au hafai ili kama hafai iwape nafasi ya kumuuondoa.
Lakini pia amewambia kuwa kwa watakao kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa maadili mwaka mzima ukiisha uwezekano wa kuwaongeza mda utakuwepo.
Naye Mwanasheria wa Halmashauri Ndg. Muyengi Muyengi amesema kuwa yeye kama mwanasheria atahakikisha kila anayekusanya mapato ya Halmashauri anakusanya kwa kuzingatia makubaliano na kwa atakayekiuka atakuwa mtu wa kwanza kusurutishwa kwa waaajili pamoja na vyombo vya Sheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa