Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Abdalla Shaib Kaim ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyokaguliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2023
Akizungumza wakati wa kuzindua Mradi wa Maji Butembo, uliopo kata ya Bureza uliogharimu Tsh. milioni 986.9 Ndg. Abdalla Shaib Kaim amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha ili kuwaletea maendeleo wananchi.
“Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 umefika katika mradi huu, umepokea taarifa ya mradi, ukakagua nyaraka na kisha kujionea kazi kubwa ambayo imefanyika. Ninayo kila sababu kuishukuru na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri inayoendelea kuifanya ikiwa ni pamoja na miradi mikubwa ya kimkakati kama mradi huu wa maji,” ameeleza Ndg. Abdalla Shaib
Aidha, ametoa salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi kuwa kupitia mradi huo wa maji wamesogezewa huduma ya maji safi na salama kwa nia na lengo la kumtua mama ndoo kichwani.
Bi. Nadhifa Yusuphu mkazi wa kijiji Butembo, kwa niaba ya wananchi wa Kijiji hicho na Kata ya Butembo ameshukuru Serikali kwa mradi huo ambao umekuwa mkombozi kwa wana Bureza kwani kwa miaka mingi walikuwa na changamoto ya kupata maji safi na salama lakini kupitia mradi huu wamepata maji safi na salama.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2023, kwa Wilaya ya Muleba umekagua, umetembelea umeweka mawe ya msingi na kuzindua jumla ya miradi yenye thamani ya Tsh. bilioni 2.
Miradi iliyokaguliwa, kutembelewa, kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa ni Mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti 500 shule ya Sekondari Nyakabango uliogharimu Tsh. milion 2, Mradi wa kikundi cha Vijana Tuinuane Seremala wenye thamani ya Tsh. milioni 32.5, Mradi wa barabara ya Shuriza-Usalama km 0.7 uliogharimu Tsh. milion 337.4.
Mradi wa Ukarabati na upanuzi wa Soko kuu Muleba Mjini uliogharimu Tsh. milioni 180.97, Mradi wa Jengo la Dharula Kituo cha Afya Kaigara uliogharimu kiasi cha Tsh. milioni 350 na Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya Sekondari Bureza vilivyogharimu Tsh. milioni 60.
Aidha Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 umetembelea Ofisi ya Kijiji Kikuku iliyozinduliwa na mwenge wa Uhuru mwaka 2022 ili kuona uendelevu wa mradi huo uliogharimu Tsh. milioni 52.8. Pia Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ulikagua shughuli za Mapambano dhidi ya Malaria, Mapambano dhidi VVU, Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya Madawa ya Kulevya na Shughuli za Lishe.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa