Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wanawake wa kijiji Kitoko, Kata Mubunda wameeleza kuwa wao ni nguvu kubwa katika kuelekea uchumi wa viwanda ambapo wamejipanga kuanzisha viwanda mbalimbali kupitia ujasiliamali wanaoufanya ikiwemo viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza batiki, ushonaji, sabuni, mafuta ya kupikia na mikoba ya akina mama .
Akieleza wakati maadhimisho hayo, Bi Alfredina Gasper, mkazi wa kijiji Kitoko amefafanua kuwa wanawake wana sanamoyo katika uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo kama ilivyo kauli mbiu ya "Kuelekea uchumi wa viwanda, Tuimarishe usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa wanawake vijijini". Hivyo wanawake wa kijiji Kitoko wamejipanga kutekeleza kauli mbiu hii kwa vitendo hivyo serikali iwawezeshe katika kuwapa mitaji.
Akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba, ASI Benjamin Mwikasyege, amewasisitiza na kuwasihi wanawake kuunda vikundi vya ujasiliamali na kuvisajili kwa ajili ya kupata mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na serikali kupitia Halmashauri. Hii ni kulingana na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ya kuwawezesha wanawake na vijana kwa kuwatengea asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Maadhimisho haya yamefanyika katika kijiji cha Kitoko, Kata Mubunda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakuu wa idara za halmashauri na Taasisi za Serikali, wawakilishi wa mashirika na wadau mbalimbali.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa