Wananchi wa Kijiji cha Kiteme na Kijiji cha Kiguzi Kata Kasharunga ambao Mradi wa Bomba la Mafuta unapita kwenye maeneo yao wamekabidhiwa nyumba rasmi zilizojengwa na kuhamia katika makazi mapya katika Kijiji cha Nkomelo Kata Kasharunga Wilayani Muleba.
Akizungumza baada ya Kukabidhiwa nyumba mmoja wa wanufaika wa Mradi huo Ndg. Saidi Ramadhani amesema kuwa kupitia mradi huo amepata manufaa ikiwa ni pamoja na Nyumba aliyokabidhiwa na familia yake imeweza kupata mahala pazuri pa kuishi tofauti na walipokuwa wakiishi awali.
Naye Bi. Evangelina Saidi ameeleza kuwa hapo awali katika eneo alilolotoka ambalo mradi unapita katika eneo hilo walikuwa wakiishi maisha ya kawaida tofauti na sasa ambapo amesema kuwa mpaka hivi sasa wameweza kufuga na kufanya shughuli mbalimbali kutokana na manufaa ya mradi huo.
"Sasa hivi nimenunua Ng'ombe watano na pamoja na mbuzi na nimeweza kumpeleka mtoto wangu Chuo cha Veta haya yote ni miongoni mwa manufaa niliyoyapata kupitia mradi huu wa Bomba la Mafuta" amesema Bi Evangelina Saidi.
KwaupandewakeBi.EneriethaWilliamKatibuwaBombalaMafutaHalmashauriyaWilayayaMulebaamewasihikuendelezamahusianomazurinamajilanizaonaendapowakipatachangamotoyeyotewasisitekuwashirikishaviongozilakinipiaamewasihikuhakikishawanalimamazaoambayoyatawasaidiakupatachakulakwaajiliyafamiliazao.
Aidha, Mratibu wa Fidia katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ndg. Kasiani Ninga ameeleza kuwa Nyumba zinazokabidhiwa kwa wananchi kama fidia ya kuhama kwenye maeneo yao ya awali kupisha mradi zimejengwa kwa kiwango zikiwa na huduma ya jiko, tenki la maji, umeme wa mionzi ya jua pamoja na huduma ya choo.
Naye Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Eng. Zefania Chacha amepongeza kwa ujenzi wa Nyumba hizo kwa kiwango kinachoridhisha na kuwasisitiza wananchi wanaohamia kwenye nyumba hizo kuhakikisha wanazitunza vizuri.
Mtendaji wa Kijiji cha Kiguzi Ndg. Alexsander Maxmilian amewaasa Wananchi waliokabidhiwa nyumba na kuhamia katika Kijiji cha Nkomelo wakae kwa amani katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nkomelo na kuhakikisha wanazitunza Nyumba zao ili waweze kukaa kwa mda mrefu.
Nyumba zilizokabidhiwa ni jumla ya Nyumba 9 kwa wananchi Saba na Nyumba hizo zote zimekabidhiwa zikiwa zimekamilika zikiwa na huduma ya matenki ya maji, vyoo, umeme wa mionzi ya jua pamoja na huduma ya Majiko ya Kupikia.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa