Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila katika siku ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria iliyofanyika katika mahakama ya wilaya amewaomba wanachi wa wilaya ya Muleba kuitumia wiki ya sheria ili waweze kupata msaaada wa kisheria ili kuweza kutatua chngamoto mbalimbali ambazo zinawasumbua kwa mda mrefu.
Akizungumza katika uzinduzi wa maadhimishi hayo amewasihi sana wananchi kwenda na kutoa ushirikiano wa kisheria kwa kupeleka shida zao za kisheria ili waweze kusaidiwa kwa kuwaeleza kuwa wapo baadhi ya watu wanadhurumiwa lakini kutokana na kutopata msaada wa kisheria lakini kama wangekuwa wanapata msaada wa kisheria huenda wasingekuwa wanadhurumiwa.
“Wiki hii itumike kama mkombozi wa maisha yetu, wiki hii itumike kama mkombozi katika kuhakikisha wananchi wetu wanapata haki, wiki hii itumike kama mwarobaini wa matatizo mbalimbali kwenye jamii yetu inawezekana na sisi wananchi tujitokeze tutumieni wakati huu ili kuweza kupata haki ili tunavofika kwenye kilele cha maadhimisho iwe ni tathmini ya yaliyofanyika kwenye wilaya” amesema Mhe. Toba Nguvila.
Lakini pia amewaomba mahakimu kuhakikisha wanatenda haki kwa kuwaeleza kuwa wasipotenda haki watakuwa hawaponyi Taifa kwasababu wakiamua tofauti na misingi ya haki maana yake mwananchi ataendelea kuumia kutafta haki yake ya msingi.
Ameongeza kwa Kumuomba Mhe.Asha Mwetinde Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya kuitumia hii wiki ya sheria kuwasaidia akina mama wajane na kumsisitiza kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kushiriki katika wiki ya sheria ili waweze kutoa dukuduku zao kuweza kupata ushauri wa kisheria.
“Wajane wanateseka sana na mirathi jamii inafanya kuwadhurumu haki zao na wanadhurumiwa kwa sababu hawajui sheria unamkuta mjane anapoteza maisha kwa sababu ya masononeko na machungu ya kunyimwa haki” ameesema Mhe Mkuu wa wilaya.
Sambamba na hayo amewaomba wananchi kuitumia tovuti ya mahakama kusoma sheria ili kuweza kuwasaidia kuzijua sheria kupitia mtandao kwa kuwaeleza kuwa ziko sheria nyingi zimewekwa kwenye tovuti ya mahakama.
Kwa Upande wake Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Muleba Mhe. Asha Mwetinde ameeleza kuwa watakuwa na siku saba kwa ajili ya kuwafikia wananchi na jamii kwa ujumla katika sehemu zao ili kuwapa elimu juu ya sheria kwa kuwaeleza huduma zinazotolewa na Mahakama pamoja na maboresho yake yanayoendelea katika muhimili huo.
Lakini pia ameongeza kwa kusema kuwa itakuwa ni fursa kwa Mahakama ya Tanzania kupata mrejesho wa huduma zinazotolewa kwa maana ya maoni maralamiko mapendekezo kwa lengo la kuyapatia ufafanuzi utatuzi lakini pia kuyawekea mipango ya kuboresha ili kuleta tija kwenye huduma zinazotolewa na mahakama ya Tanzania.
Naye miongoni mwa wananchi waliohudhulia maadhimisho hayo Ndg. Pastori Ihinduka amependekeza wazeee wa mabaraza ya kata wanapoteuliwa wapewe semina ya namna ya kuendesha mabaraza kwa haki.
Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Zama za Mapinduzi ya Nne ya viwanda safari ya maboresho kuelekea mahakama mtandao” Ikiwa na lengo la kuwasaidia wananchi kuweza kupata huduma za kisheria kimtandao kwa kuwasaidia wananchi kufungua kesi zao kwa njia ya kimtandao na kesi yake kuchakatwa kimtandao ili anayehusika aweze kupata taarifa bila yeye kufika mahakamani.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa