Katika maadhimisho ya Miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Muleba Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera Mhe. Nazir Karamagi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Abel Nyamahanga kusimamia mradi wa maji Kyamyolwa ili uweze kumalizika kwa wakati na kuanza kutumiwa na wananchi.
Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua Mradi huo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa amemuagiza Mkuu wa Wilaya kuhakikisha kabla ya ya mwaka haujaisha mradi huo uwe umekamilika na kuanza kutumiwa na wananchi.
"Kabla ya mwisho wa mwaka tutakuja tena kukagua na kujihakikishia kama mradi umekamilika watu wawe wanakunywa maji salama kuna kaya zaidi ya elfu kumi na nne kata zaidi ya tatu zinazotegemea haya maji hivyo ni vema huu mradi ukamilike ili uwanufaishe wananchi" amesema Mhe. Nazir Karamagi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Abel Nyamahanga amemuhaidi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kuwa atahakikisha anasimamia mradi huo kwa kushirikiana ma Meneja pamoja na Mkandarasi ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati kama Mwenyekiti alivyoelekeza.
Katika Taarifa iliyosomwa na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Muleba Eng. Patrice Jerome amesema kuwa mradi huo utazihumia kata tatu kata ya Kasharunga, Bisheke na Rulanda pamoja na vijiji vya Kyamyolwa, Rulanda na Kabuga hivyo utawanufaisha zaidi ya watu 13,860 pamoja na taasisi nne za Umma.
Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za benki ya Dunia chini ya programu ya lipa kwa matokeo ijulikanayo kama (PforR) mpaka kukamila mradi utagharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 3.7
Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa