MKUU WA WILAYA MTEULE WA WILAYA YA MULEBA AKABIDHIWA OFISI RASMI.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dkt Abel Mwendawile Nyamahanga aliyeteuliwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 25.01.2023 amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Kemirembe Rwota leo tarehe 30.01.2023.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Muleba ameiomba kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya kuhakikisha wanampa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kuyatimiza majukumu yake ya kazi na matakwa ya wananchi.
"Tusimamie tushiriki watu wafanye kazi ili maendeleo yaweze kupatikana kwa ajili yao wananchi wenyewe na kwa manufaa ya Serikali kwa ujumla" amesema Mhe. Dkt Abel Mwendawile Nyamahanga.
Aidha, Amewasihi kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha wanailinda amani katika Wilaya ya Muleba ili watu waweze kufanya shughuli zao za maendeleo kwa amani na utulivu bila ya kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani.
Naye, Mhe. Kemirembe Rwota aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Muleba amemueleza kuwa wakaziwaWilayayaMulebawanajishughulishanashughulizaKilimo,UfugajinaUvuvi na ina jumla ya Kata 43 vijiji 166 na vitongoji 752 pamoja na visiwa 39 ambapo jumla ya visiwa 25 ndo visiwa vyenye wakazi.
Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa