Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila amezindua rasmi ujenzi wa Hospitali ya wilaya inayojengwa katika eneo la Marahala wilayani Muleba na kuwahimiza mafundi kujenga na kumaliza haraka ndani ya mwezi mmoja.
Akizungumza katika uzinduzi huo amesema kuwa kazi ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ni lazima ifanyike usiku na mchana ili kumaliza haraka na kumuhimiza mhandisi kufika eneo la ujenzi kusimamia ubora wa ujenzi ambao unakidhi viwango
"Idadi ya mafundi hapa iongezeke mala dufu fundi mkuu ni lazima uajiri mafundi wengi wa kutosha ili kazi ifanyike usiku na mchana na vifaa visikosekane hatutaki kusikia kuna upungufu wa tofari kwa sababu fedha zipo kwenye akaunti anapofanya kazi hatua flani fundi alipwe fedha zake" amesema Mhe Toba Nguvila.
Aidha, Mkuu wa wilaya ameongeza kwa kusema kuwa wananchi wa Muleba wananenda kunufaika na ujenzi wa Hospitali ya wilaya kwa kueleza kuwa baada ya ujenzi kukamilika na hospitali kufunguliwa wananchi wataweza kupata huduma bora kwa uharaka na kwa unafuu na kuwasaidia kuwapunguzia gharama za matibabu ambazo walikuwa wanazitumia katika hospitali teule ya Rubya.
Sambamba na hayo ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa utoaji wa fedha za ujenzi wa hospitali ya wilaya kwa kutambua na kuona umuhimu mkubwa kwa wananchi wa wilaya ya Muleba kupata hospitali ya wilaya.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Muleba Ndg. Greyson Mwengu ametoa pongezi kwa Mhe Rais kwa utoaji wa fedha za ujenzi wa hospitali hiyo na kuhaidi kuwa watasimamia kuhakikisha ujenzi unamalizika kwa wakati kwa kuzingatia ubora.
Naye Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilayani Muleba Ndg. Athuman Kahara ametoa shukrani kwa Mhe.Rais kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya na kuhaidi kuwa watahakikisha wanajenga kwa uharaka kama walivyojenga madarasa ya uviko 19 ili kumaliza kwa wakati.
Katibu Afya wa wilaya ya Muleba Ndg. Auxsilius Mathew ameeleza kuwa wananchi walikuwa wanapata changamoto za matibabu kutokana na kutokuwepo kwa hospitali ya wilaya ambapo ameeleza kuwa wananchi walikuwa wanapata matibabu kwa gharama kubwa kwenye hospitali binafsi lakini ikishakamilika hospitali ya wilaya gharama zitakuwa ziko chini na wananchi wataweza kuzimudu.
Fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ni kiasi cha shilingi milioni 500 na majengo yatakayoanza kujengwa ni jengo la OPD kwa ajili ya wagonjwa wa nje na jengo la maabara ambapo majengo yote hayo mawili ndio yatajengwa kwa kiasi cha Tsh. Milioni 500
Imeandaliwa na Kutolewa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa