Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dr Abel Nyamahanga amewasihi wazee kushirikiana na viongozi wa Dini kuendelea kuitunza na kuilinda amani ndani ya Wilaya ya Muleba alipokutana nao leo na kufanya kikao katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya amewasihi wazee kwa kushirikiana na viongozi wa dini kuhakikisha wanakaa na kuwaonya vijana juu ya mwelekeo mzuri wa namna ya kuishi kwa kuifuata mienendo inayostahili katika jamii pasipo kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani.
"Wazee kwa kushirikiana na viongozi wa Dini mnaomchango mkubwa sana katika kuitunza na kuilinda amani na jamii bado inawaheshimu sana wazee na viongozi wa Dini bado hiyo hadhi haijapotea kwahiyo ni jukumu letu kuilinda amani katika maeneo yetu" amesema Mhe. Dr Abel Nyamahanga.
Aidha, amewasihi wazee kuwa ni jukumu lao kuhakikisha wanazitunza na kuzirithisha mila na desturi zilizonjema kwa vijana wa kizazi cha sasa na cha baadae ili ziweze kuwasaidia katika maisha yao.
Sambamba na hayo amewahimiza pia wazee kuwahamasisha vijana kuhusu umuhimu wa kufanya kazi ambapo amewaeleza kuwa ni muhimu vijana wasikae mtaani bila kufanya kazi ni vema wakajihusisha na kazi mbalimbali kwa ajili ya kuongeza kipato chao na kumudu gharama mbalimbali za maisha.
Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa