Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dr Abel Nyamahanga ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera kupitia idara ya elimu Sekondari kufanya uhamisho wa aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Kimwani Mwl. Peter Jovin kuhamishiwa shule nyingine kwa kosa la kutuhumiwa kutembea na wanafunzi katika shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na walimu wa shule hiyo ya Kimwani baada ya baadhi ya wazazi kulalamikia kitendo cha mwalimu huyo kushushwa cheo cha Ukuu wa shule na kuendelea kubaki shuleni hapo.
"Ni lazima mwalimu huyu aondoke katika kituo hiki haraka iwezekanavyo, atoke kwa masilahi ya taasisi kitendo cha kutuhumiwa kwa kosa la kutembea na wanafunzi ni kosa kubwa sana" amesema Mhe. Dr Abel Nyamahanga.
Aidha, amesema kuwa kitendo cha mwalimu huyo kubaki shuleni kinaweza kikawafanya wanafunzi kushindwa kukaa kwa amani shuleni hapo hivyo ameagiza mwalimu huyo ahamishwe pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa ya tuhuma inayomkabili.
Sambamba na hayo amewasihi walimu kuwa ni mienendo mizuri wawapo shuleni ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawalea vizuri wanafunzi wanawatunza na kuwapa elimu bora na kuwa mifano ya kuigwa kutoka kwa wanafunzi wanaowafundisha.
Kwa upande wake Afisa elimu Sekondari Wilaya ya Muleba Mwl. Jaredi Muhile amesema wahakikisha wanalifanyia kazi agizo hilo la kumuhamisha mwalimu huyo kutoka shuleni hapo na kumtaftia shule nyingine.
Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa