Katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kimkoa Wilayani Muleba Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila amehaidi kudhibiti vitendo vya kikatiri dhidi ya wanawake na watoto ambavyo vinaweza kusababisha kushindwa kupata haki zao za msingi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa amesema kuwa miongoni mwa vitendo vya kikatiri ni vipigo, mauaji, kubakwa pamoja na ndoa za utotoni hivyo atahakikisha vitendo hivyo vinadhibitiwa kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji hadi Mkoa.
" Wanawake muendelee kuwa wajasiri ili msinyanyasike na waume zenu lakini pia hata jamii zetu kizazi hiki ambacho kinaendelea kukua ili kesho wawe viongozi hawa tunahitaji msingi mkubwa wa malezi unaotolewa na mwanamke leo hii mashuleni tunapiga kelele na mwanamke kwa matendo haya ya ukatili kwa wanawake, ukatili wa wasichana na hata kwa watoto wadogo" amesema Mhe. Albert Chalamila.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dr Abel Nyamahanga amesema kuwa vitendo vya vurugu vinavyoashilia uvunjifu wa amani vikifanyika akina mama na watoto ndio wanakuwa wa kwanza kuumia hivyo amehaidi kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote watakaoshiriki kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani hasa kwa wanawake.
Katika Risala iliyosomwa na Afisa Afya na Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kagera Bi. Aisha Dallu amesema kuwa katika utoaji wa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri vikundi vya wanawake vilivyopo Mkoani Kagera kwa mwaka wa fedha 2021-2022 hadi kufikia mwezi wa Sita mwaka 2022 kiasi cha Tsh. Bilioni 2.24 kilikopeshwa kwa vikundi 236 kwenye Halmashauri za Mkoa wa Kagera.
Naye Newaeli Nestrome Mfanyakazi wa Shirika la MDH amesema kuwa wao katika maadhimisho ya siku hiyo wameweza kujikita katika kuhamasisha wanawake wote ambao wanafanyiwa vitendo vya kikatili kuweza kuhudhulia katika vituo vya afya ambapo watapatiwa utambuzi pamoja na huduma za matibabu wamewahamasisha wanawake waweze kuchunguzwa saratani ya shingo ya kizazi ili waweze kutambua afya zao.
Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa