Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, amekutana na Wakuu wa Idara na Vitengo Pamoja na Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali Wilaya ya Muleba ili Kujadili na kuweka maadhimio mbali mbali na mpango mkakati wakuondoa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa viti na madawati Wilayani humo.
Akizungumza katika kikao Mkurugenzi Mtendaji Dkt,Peter Nyanja amewataka walimu wote wa Shule za Sekondari kuweka mkakati wa haraka na kuhakikisha ifikapo Januari,2024 tatizo la uhaba wa Viti na Madawati linamalizika Wilayani Muleba.
"Kumekuwa na tatizo la uhaba wa Viti na meza kwenye baadhi ya shule hivyo nimewaita hapa walimu Wakuu wote ili tujadili namna ya kumaliza Changamoto hii kwenye Shule zetu"
Aidha, Dkt. Nyanja alitumia muda huo kuwakumbusha walimu kutojihusisha na wizi wa Mitihani kwani wizi ni jambo la aibu na halikubaliki.
"Lipo tatizo kubwa la wizi wa Mitihani kwa kushirikiana na wasimamizi wa mitihani hivyo naagiza tabia hii iachwe Mara Moja"
Sambamba na hilo, Dkt.Peter Nyanja,alitumia kikao hicho kuwasihi walimu kuacha tabia ya matumizi ya pombe wawapo Kazini kwani nikinyume cha maadili ya kazi kwa mtumishi wa umma.
Naye, Kaimu Afisa Elimu Sekondari, Mwalimu Masatu Bwire amesema kuwa zaidi ya wanafunzi 18105 wanatarajia kuanza Kidato Cha kwanza Mwezi Januari, 2023 katika shule zote za serikali zilizopo Wilaya ya Muleba kati yao Wasichana ni 9344 na Wavulana 8761.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali Wilayani Muleba Mwalimu Venance Nzahaebona amewashauri walimu kufanya matengenezo ya Viti na meza vilivyoharibika ili viweze kuwasaidia Wanafunzi wanaotarajia kuanza masomo Januari,2024.
"Kwa upande wangu mimi nimesha fanya matengenezo ya Viti vyote na Meza hivyo ni vyema tuanze kutengeneza tunapoendelea kufanya Utaratibu wa kumaliza tatizo hili"
Aidha ,Mwalimu Benetson Mpanju Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyakatanga amewashauri Wajumbe wa kikao hicho kufanya vikao baina ya Walimu,Menejimenti ya Shule pamoja na Wazazi ili kutafuta Mwarobaini wa changamoto ya madawati,viti na changamoto Nyingne zinazo weza kuathiri Maendeleo ya Mwanafunzi ifikapo Januari, 2024.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu: 0744644702
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa